MATUTA YAIONDOA KILIMANJARO STARS KOMBE LA CHALENJI
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kimeng’olewa katika michuano ya
Chalenji baada ya kufungwa katika mechi ya robo fainali kwa mikwaju ya penalti
4-3.
Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia nahodha
wake, John Bocco lakini wenyeji wakasawazisha kwa mkwaju wa penalti baada ya
Shomari kapombe kumuangusha mshambuliaji wao.
Katika mikwaju ya penalti, Kili Stars ilipoteza penalti
kupitia kwa Jonas Mkude kabla ya Shomari Kapombe naye kupoteza zote
zikipanguliwa na kipa wa Ethiopia.
Kili Stars ilikuwa na nafasi zaidi ya kushinda baada ya
kpata nafasi nyingi zaidi za kufunga ikiwemo ile ya Said Ndemla aliyeshindwa
kuitumia akiwa amebaki na lango tu.
Kili Stars inayonolewa na Abdallah Kibadeni ilishambulia
mara 15 katika kipindi cha kwanza huku wenyeji Ethiopia wakishambulia mara 6 tu.
Suala la kupoteza nafasi, limechangia kuiondoa Stars katika michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment