CCM YAKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI KWAMBA IMEKUBALI KUMKABIDHI MAALIM SEIF IKILU
Na Maelezo Zanzibar 30/11/2015
Chama cha
Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii
kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim
Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano.
Akikanusha
Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi
uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla.
Amesema
toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa
ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo.
“Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai.
Amesema
kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama
ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa
upya.
Aidha
Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na
wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na
kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria.
“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai.
Katika
taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema
kuwaChama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif
Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na
yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika
kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa
makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri.
Vuai
amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa
kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi
kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
0 comments:
Post a Comment