Thursday 5 November 2015

PICHA::: DK JOHN POMBE MAGUFULI ALIVYOKULA KIAPO KUWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.               

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA