Monday, 30 November 2015

RC KILIMANJARO AKUTANA NA WATENDAJI WA SERIKALI KATIKA KIKAO CHA UTENDAJI KAZI

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Amosi Makala akizunumza na wakuu wa wilaya ,wakurugenzi,Wakuu wa taasisi mbalimbali za umma katika kikao cha utendaji kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho,kutoka kuslia ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka, Helman Kapufi (Mkuu wa wilaya ya Same) Novautus Makunga (Mkuu wa wilaya ya Moshi) na Lembris Kipuyo (Mkuu wa wilaya ya Rombo).
Baadhi ya wakurugenzi wakiwa katika kikao hicho.
Watendaji wengine wa serikali wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao .
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Severine Kahitwa akizungumza katika kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya watendaji wa taasisi za umma,kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru.
Badhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.


KATIKA kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli ya “Hapa Kazi tu” serikali mkoani Kilimanjaro imetangaza kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika kipindi cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.

Agizo hilo linakuja wakati tayari baadhi ya watumishi wa serikali kuanza taratibu za kuomba likizo na ruhusa kwa ajili ya kwenda kushiriki siku kuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.

.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala alitangaza uamuzi huo jana wakati wa kikao  cha kazi alichoitisha na wakuu wa wilaya zote za mkoa, wakurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na watendaji wengine wa serikali.

 “Mh Rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika,Makamau wa rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika ,Waziri mkuu pia vivyo hivyo sasa sisi  ni nani twende kwenye mapumziko ya siku kuu ya Krismasi.”alihoji Makala.

“Kwa maana hiyo ili haya tunayotaka ya elimu bure ,kukabiliana na Kipindupindu ,kwa madaraka niliyopewa kama mkuu wa mkoa nasitisha likizo zote,kwa Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi na wakuu wote wa idara ili mambo haya yaweze kutekelezwa,tumesema Hapa ni kazi tu”aliongeza Makala.


Alisema utekelezaji wa agizo la rais la kufanya usafi siku ya sikuu ya Uhuru inayofanyika Desemba 9 kila mwaka ,mapambano ya ugonjwa hatari wa Kipindupindu ambao umeendelea kusambaa sehemu kubwa ya nchi hayawezi kusubiri hadi watusmishi wa serikali watoke likizo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA