STOKE CITY YAZIDI KUZAMISHA JAHAZI LA CHELSEA LIGI KUU

Mdudu wa vipigo ameendelea kuiandama Chelsea baada ya kufungwa tena leo katika Ligi Kuu England baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 dhidi ya Stoke City.
Kipigo hicho kinaifanya Chelsea kuwa imepoteza mechi ya 7 kati ya mechi 12 ilizocheza. Jambo ambalo halikuwahi kutokea kwa bingwa kufungwa mfululizo mechi na mwisho idadi kufikia mechi 7.

Kinda Jesse Lingard amefunga goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuisaidia Manchester United kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Old Traffiord.
Jesse Lingard alipachika bao hilo zuri katika dakika ya 52, kwa shuti la kuzungusha, ambapo Juan Mata alipachika goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Anthony Martial, kuchezewa rafu na Gareth McAuley aliyepewa kadi nyekundu kwa kosa hilo.
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza ni, Bournemouth 0 - 1 Newcastle, Leicester 2 - 1 Watford, Norwich 1 - 0 Swansea, Sunderland 0 - 1 Southampton na West Ham 1 - 1 Everton.
0 comments:
Post a Comment