URAFIKI NI "NIPE NIKUPE" ,SOMA HAPA UPATE KITU
Siku hizi huku kwenye mitandao watu wana maneno na misemo ambayo wakati mwingine ukifatilia ni kweli tupu
.Haya maneno ni kweli kabisa kuna wakati nilikuwa hivyo.Unaweza kuwa una marafiki wewe kichwani kwako unadhani ni watu wako kumbe walaaa.Sasa kwasababu una nia safi nao unajikuta kila siku wewe ndio uwasabahi,uwatafuta na bado wasipatikane yaani watakuwa karibu na wewe kwa sababu ya situation flani inayomuhusu yeye akipita hiyo hali humuoni ng'oo.
Au anakuwa karibu na wewe aliakamilishe kitu flani akikamilisha humuoni unabaki wewe kumtafuta atakupa sababu laki 8 za kwa nini siku hizi humuoni.Kuna watu watakuwa karibu na wewe ili akufanye ngazi ya kupanda mahali flani akishapanda anakutupa kule.Mifano ni mingi sana ambayo hata wewe mdau unaweza kuongezea.
Nilipokutana na huo msemo nikasema ngoja niuweke hapa inawezekana kuna mtu mwingine nae haya yanamfika.
Ndio maana nimesema Urafiki ni Nipe Nikupe..kila mmoja akiutambua wajibu wake kila kitu kitaenda sawa.