Thursday, 26 November 2015

WAKAZI WA MIKOA YA MANYARA,ARUSHA NA KILIMANJARO WAJITOKEZA UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .
Wanafunzi wa kozi ya awali ya Askari Polisi kutoka shule ya Polisi Tanania wakiwa katika manda,ano ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini.
Maanda,mano ya lipita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
Maandamano hayo yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi yakieekea katia viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini .
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kujinsia kanda ya kaskazini akimsikiliza Mwenyekiti wa Mwavuli wa Vikoba wa KIVINET ,Mama Mwingira wakati alipotembelea banda la KIVINET .
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukeketaji.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiiza maelezo kutoka TAWREF ambao pia wameshiriki katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Velonica Ollomi akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi,kulia kwake ni Afisa Kitengo cha elimu ya haki za binadamu na jinsia ,KWIECO ,Elizabeth Mushi.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA ,pia imeshiriki katika uzinduzi huo hapa ikiwasilishwa na afisa habari wake,Florah Nguma na mfanyakazi wa mamlaka hiyo,Kisingi.
Mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini,Honorata Nasuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Kikundi cha kwaya kutoka shule ya msingi Mweleni wakitoa ujumbe kwa njia ya wimbo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini.
Mkurugenzi wa shirika la Tusonge,Agnata Rutazaa akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa TAWREF,Dafrosa Itemba akitoa mada katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.
Mkurugenzi wa shirika la KWIECO,Elizabeth Minde akitoa mada katika uzinduzi huo.
Mwakilishi wa mkuu wa shule ya Polisi Tanzania na Mkufunzi mkuu wa shule hiyo Graifton Mushi ,akiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa dawati la Jinsia mkoa wa Kilimanjaro,Grace Lyimo katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la KWIECO,Elizabeth Minde.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga aliyekuwa mgeni trasmi katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini akitoa hotuba yake.
Baadhi ya wasiriki katika uzinduzi huo wakifutilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA