CAPITAL ONE CUP: LIVERPOOL YATINGA NUSU FAINALI KWA KISHINDO
Timu ya Liverpool imekua timu ya
mwisho kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi
maarufu kama Capital one .
Liverpool wamefanikiwa kusonga kwa hatua hiyo baada ya kuichapa timu ya Southampton kichapo cha mabao 6-1.
Southampton walianza kuandika bao la mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Sadio Mane.
Liverpool
wakachomoa bao hilo kupitia mshambuliaji wao Daniel Sturridge katika
dakika ya katika dakika ya 29 , Sturridge, tena akaongeaza bao la pili.
Mshambuliaji
Divock Origi akaongeza mabao mengine matatu katika dakika ya 45, 68,
86, huku Jordan Ibe nae akifunga bao moja, na kukamilisha idadi ya mabao
6.
Michezo ya nusu fainali ya kwanza itafanyika January 5 na 6 na
michezo ya marudio ikifanyika 25 na 26 ambapo Liverpool watachuana na
Stoke City katika mchezo wa nusu fainali huku Manchester City wao
wakikabiliana na Everton.
PICHA NA BBC
0 comments:
Post a Comment