Thursday 31 December 2015

HOFU YA KUSHAMBULIWA: UBELGIJI YAAHIRISHA FATAKI USIKU WA MWAKA MPYA

Ulinzi umeimarishwa Brussels

Ubelgiji imesitisha sherehe za kijadi za kuwasha fataki mjini Brussels katika mkesha wa mwaka mpya, kwa hofu ya shambulizi.

Meya wa mji wa Brussels, Yvan Mayeur, amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kufanywa kwa tathmini.
Mwanzoni mwa wiki hii, watu wawili walikamatwa nchini humo kwa kushukiwa kutaka kupanga shambulizi mjini Brussels katika mkesha wa mwaka mpya.
Ubelgiji imekuwa katika tahadhari ya hali ya juu tangu kutokea kwa shambulizi la kigaidi nchini Paris mwezi uliopita.
Baadhi ya wanaoshukiwa kuhusika na shambulizi hilo wapo nchini Ubelgiji.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA