Tuesday 22 December 2015

RAIS OBAMA AZUNGUMZIA UGAIDI

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani amekubali kutoweka bayana mipango ya serikali yake katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani na hasa kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam maarufu kama Islamic State.
Amesema kwamba ikiwa watu hawafahamu juu ya maelfu ya mashambulio ya anga yanayoongozwa na majeshi ya Marekani na washirika wake dhidi ya wanamgambo hao, basi watakuwa na mashaka kwa kile kilichokwisha fanyika na kwamba juhudi hizo hazijatosha.
Rais Obama alitoa tamko hilo katika mahojiano ya wazi yaliyofanywa mwanzoni mwa wiki hii akiwa mapumzikoni nje ya nchi yake; yeye na familia yake katika visiwa vya Hawaii.
Rais Obama hakusita kuelekeza shutuma zake kwa mgombea wa chama cha Republican anayegombea nafasi ya urais, Donald Trump kwa kuleta mkanganyiko pamoja na kuzidisha wasiwasi na kuwataka wanaume waliostaarabika na wenye elimu ya kutosha kuongeza nguvu katika kampeni za mgombea huyo.
Trump aliwahi kutoa wito wa kuzuiliwa waisilamu kuingia nchini Marekani baada ya shambulio la hadhara mjini California lililosababishwa na wapenzi wawili wanaoaminika kuwa ni watu waliokuwa na msimamo mkali.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA