Monday 21 December 2015

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA VITENDO

Mnyama Ngiri akiwa amejipumzisha kwenye tope kama alivyokutwa na kamera yetu
Baadhi ya Wanafunzi  wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanya ziara ya siku mbili ya kitalii katika hifadhi ya taifa ya Saadani pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.


Wanafunzi hao kutoka katika "Collage" tofauti tofauti ikiwemo utalii , uchumi na biashara waliofanya ziara hiyo ikiwa chini ya mwamvuli wa University of Dar es Salaam Tourism Association (DUTA) ,walipata fursa ya kujifunza na kushuhudia wanyama pori pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole na kuhamasisha jamii hasa ya wasomi kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzuru hifadhi pamoja na makumbusho ili kuhimiza utalii wa ndani.
Hii ni tabia ya kipekee ya ngiri ambapo hula nyasi akiwa amepiga mfano wa magoti kwa kukunja miguu ya mbele
Waterbucks kama wanavyojulikana wakiwa miongoni mwa wanyama walioonekana wakati wa ziara hiyo


Akizungumzia ziara hiyo aliyekuwa kiongozi wa msafara huo  ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya utalii ,Gabriel Lyimo alisema huu ni muendelezo wa ziara ambazo wamekuwa wakizifanya kama sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha watanzania na hasa wanafunzi pamoja na wasomi kujenga utamaduni wa kukuza pato la taifa kwa kufanya utalii wa ndani na sio kuona kama ni jukumu la wageni.
Picha ya pamoja

Sambamba na hilo wanafunzi hao walipata fursa ya kuweka kambi pembezoni mwa mwambao wa bahari ya hindi na kutumia fursa hiyo kupata upepo mwanana , kupumzika na kuogelea.


Saadani National Park ni Hifadhi ya Taifa ya 13 ya Tanzania yenye  eneo la 1,062 km za mraba ambapo watalii wanaweza kuona wanyama pamoja mwambao Bahari ya Hindi.Mbuga hii ilikuwa rasmi katika gazeti la serikali mwaka 2005, Saadani National Park ni hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo imepakana na bahari ya Hindi.

Mtembezi na muelekezi katika hifadhi  ya  Saadani Bw.Mollel akifafanua jambo wakati wa ziara ndani ya hifadhi
Baadhi ya wanafunzi  wakisikiliza historia kuhusu mji huu wa Saadani huku toka kwa mwenyeji na mkongwe wa eneo hilo mzee Mlelwa (mwenye shati la kijani) wakati wa jioni
Mambo ya Msosi: baadhi ya wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchoma kitoweo kwa ajili ya mlo wa usiku 

Hakika anapendeza!!
wanafunzi hao wakiwa  karibu  na eneo ambalo maji kutoka mto wami yanakutana na maji ya bahari ya hindi

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichagua shanga na vito vya asili walipozuru Kaole Mamba Ranch iliyopo Bagamoyo
Moja kati ya mamba wanaopatikana katika eneo la Kaole Mamba Ranch
Kwa umakini na huku wakipewa fursa ya kuuliza maswali , wakisikilza historia ya eneo la Kaole na mfululizo wa matukio ya kihistoria kutoka kwa mtaalamu wa historia Bw.Ramadhani 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa mbele ya msikiti wa kwanza uliojengwa katika pwani ya Afrika ya mashariki
Kulingana na historia ya eneo hili ,inasemekana kuwa mbuyu huu umeishi zaidi ya miaka mia tano na wengi wamekuwa wakiamini kuuzunguka mbuyu huu (kutoka upande wa kushoto kwenda kulia) kunaweza kumuongezea mtu miaka ya kuishi
Picha na Dickson Mulashani wa FUNGUKA LIVE MEDIA

  1 comment:

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA