Thursday, 3 December 2015

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA TENA TPA NA TRL, ZAIDI YA MAKONTENA 2000 YALETA UTATA,MENEJA APEWA MASAA 3


Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli
(TRL) na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA