AFRIKA YA KATI MAMBO BADO! UCHAGUZI MKUU
wagombea
wa uraisi ishirini kati ya thelathini katika jamhuri ya afrika ya kati
wametoa wito wa kura zilizopigwa kufutwa kwa madai ya kuwepo kwa
ulaghai.
Matarajio
yalikuwa baada ya uchaguzi jumatano hali ya amani ingeweza kurudi
nchini humo ambako maelfu wamefariki dunia katika vita vya kidini.
kura
zaidi ya robo zimehesabiwa, waziri mkuu wa zamani , faustin archange
touadera, ndio anaongoza mpaka sasa. msemaji wa kundi la wagombea hao
ishirini , théodore kapou , amewaambia waandishi wa habari kuwa hawawezi
kukubali njia za uendeshaji uchaguzi .
"Sisi ,
wagombea kwa uchaguzi wa urais, watia sahihi wa tamko hili, tunakataa
ushirika wa uchaguzi batili kama huu, Tunatangaza kuwa mchakato wa
uchaguzi ' si wa kuaminika ' . Ni lazima usimamishwe ili ushirikiano
uwepo na utekelezwaji uendele.BBC
0 comments:
Post a Comment