GPA HAIKUWA SABABU YA KUONDOKA NECTA, PROF.NDALOCHAKO AFUNGUKA
Waziri wa
Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amesema
mfumo wa wastani wa alama za mtihani (GPA) haukuwa sabababu ya yeye
kuondoka katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA).
Prof,
Ndalichako alisema hayo wiki iliyopita wakati akijibu maswali ya
waandishi wa habari kutokana na uvumi uliozagaa mitaani ikiwemo kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa alijiuzulu nafasi hiyo kutokana na
kushinikizwa kuukubali mfumo huo.
Alisema
aliondoka NECTA baada ya kufanya kazi katika baraza hilo kwa miaka tisa,
hivyo muda huo aliona unatosha kwa yeye kuliongoza baraza hilo la
mitihani nchini.
“GPA haikuniondoa NECTA kama ambavyo nimekuwa nikisikia maneno mitaani kuwa niliondoka ili kupisha mfumo huu wa GPA kuanza kutumiwa na baraza hili la mitihani nchini,”
“GPA haikuniondoa NECTA kama ambavyo nimekuwa nikisikia maneno mitaani kuwa niliondoka ili kupisha mfumo huu wa GPA kuanza kutumiwa na baraza hili la mitihani nchini,”
Prof.
Ndalichako alisema kuondoka kwake kulisukumwa na kazi kubwa alizokuwa
amezifanya katika baraza hilo, pamoja na kuweka mifumo mbalimbali ya
kisasa katika usajili na mambo mengine ya kitaalamu ambayo hayakuwapo
kabla yake.
“Nimefika pale NECTA nikakuta kuna baadhi ya watendaji wanadai hawaejenda likizo kwa zaidi ya miaka mitatu, hii yote ilikuwa ni kutoka na mifumo iliyokuwa ikitumika ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa kwenye vichwa vya watu hivyo wao kama hawatakuwapo basi kazi nyingine hazifanyiki...nikamua kuanzisha mifumo ya kisasa na kuacha kutegemea vichwa vya watu,”

Ndalichako alisema sababu nyingine iliyomuondoa NECTA ni kutaka
kujiendeleza kielimu kutoka alipokuwa wakati huo na kupanda katika ngazi
nyingine, kwani kama angeendelea kubaki asingeweza kujiendeleza.
“Nilitoka Necta nikarudi Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu ili kujiendeleza na hivi sasa mimi ni profesa lakini nilipokuwa Necta nilikuwa dokta, hivyo hayo maeneno yanayozagaa kuwa mimi nilikimbia GPA si ya kweli hata kidogo na mfumo huo ulianzishwa mimi nikiwa sipo pale,”
Credit-NIPASHE

0 comments:
Post a Comment