MAJALIWA AONGOZA MBIO ZA HAPA KAZI TU DODOMA HALF MARATHON
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za Wabunge Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. Mwansasu.
Mmoja wa wapigapicha walioshiriki mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon alilazimika kuomba msaada kwa askari wa usalama barabarani Mjini Dodoma Januari 30, 2016..
Baadhi ya Washiriki wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon wakishiriki mmbio hizo mjini Dodoma Januari 30, 2016.(P.T)
Mbunge wa
Mbulu Vijijini,Fratei Massay akifanya mazoezi kabla ya kuanza mbio za
Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Januari 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Pikipiki mshindi wa kwanza
upande wa wanawake wa Mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon, Angela
Davile (kulia) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza
wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon upande wa wanaume,
Emmanuel Giriki kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Benki ya CRDB tawi la Dodoma ambao wamedhamini pambano la mpira wa
miguu kati ya wabunge na benki hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri Januari
30,2016. Benki hiyo pia ilitoa vifaa vya michezo kwa timu ya Bunge.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment