MIEZI MITATU KLOPP AIFIKISHA LIVERPOOL FAINALI KOMBE LA LIGI
Liverpool
wametinga Fainali ya C1C, Capital One Cup, baada ya kuishinda Stoke
City Uwanjani Amfield kwa Penati 6-5 baada ya kufungwa Mechi hiyo 1-0 na
kufanya Jumla ya Mabao kwa Mechi 2 kuwa 1-1.Bao la Soke lilifungwa
Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza na Marko Arnautovic na Matokeo
kubaki hivyo hivyo baada ya 90 kwisha na Nyongeza ya Dakika 30
kutobadili chochote.
Ndipo
zikaja Penati na Kipa wa Liverpool Simon Mignolet kuokoa Penati za Peter
Crouch na Marc Muniesa na kuifanya Liverpool, chini ya Meneja Jurgen
Klopp katika Msimu wake wa kwanza, kutinga Fainali Wembley ambako
watacheza na Mshindi kati ya Man City na Everton.
Penati za
Stoke zilifungwa na Jon Walters, Glenn Whelan, Ibrahim Affelay, Xherdan
Shaqiri na Marco Van Ginkel wakati za Liverpool zilifungwa na Adam
Lallana, Christian Benteke, Roberto Firmino, James Milner, Lucas na Joe
Allen.
+++++++++++++++++++++++
Nusu Fainali-Kanuni Muhimu:
-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.
-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.
-Ikiwa Gemu ni Sare baada ya hiyo Nyongeza ya Dakika 30, Mshindi atapatikana kwa kuhesabu Goli la Ugenini kuwa mara mbili.
-Ikiwa
Gemu bado itakuwa sawa hata baada ya kuhesabu Goli za Ugenini ni mara
mbili, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5 kama Sheria za
Soka zinavyotamka.
+++++++++++++++++++++++
VIKOSI:
Liverpool
Mignolet; Flanagan, Toure, Sakho, Moreno; Lucas, Can, Henderson; Milner, Lallana; Firmino
Akiba: Ward, Lovren, Benteke, Allen, Ibe, Teixeira, Smith.
Stoke City
Butland; Johnson, Wollscheid, Muniesa, Pieters; Whelan, Afellay; Walters, Krkic, Arnautovic; Crouch
Akiba: Bardsley, Joselu, Wilson, van Ginkel, Adam, Shaqiri, Haugaard.
REFA: Jon Moss
C1C: NUSU FAINALI:
Marudiano
Januari 26
-Liverpool 0 Stoke City 1 [1-1, Liverpool washinda Penati 6-5]
Januari 27
**Mechi zote Saa 5 Usiku, Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo katika Meichi ya Kwanza ya Nusu Fainali
-Man City v Everton [1-2]
+++++++++++++++++++++++
FAINALI
Februari 28
Liverpool v Man City au Everton
0 comments:
Post a Comment