Thursday, 21 January 2016

RAIS DK.JOHN MAGUFULI KUTUA ARUSHA KWA MARA YA KWANZA TANGU KUAPISHWA


Rais Dk. John Magufuli leo anatarajiwa  kuwasili  mkoani  Arusha ambapo kesho atakuwa  mgeni  rasmi  katika sherehe  za  kutunuku kamisheni kwa  maofisa  wanafunzi wa Chuo  cha Mafunzo  ya  Kijeshi  cha (TMA), Monduli.

Mkuu  wa  Mkoa wa  Arusha, Felix Ntibenda, alisema  Dk. Magufuli   atawasili kupitia  Uwanja  wa  Ndege  wa  Kimataifa  wa  Kilimanjaro  na amewaomba  wananchi  kujitokeza  kumpokea.

"Nawaomba sana wananchi wa Mkoa wetu kw amara ya kwanza tangu awe rais, ndio anakuja Mkoani kwetu, tujitokeze kumpokea,"alisema.

Kwa  mujibu  wa  ratiba  iliyotolewa  na  Mkuu   wa  Chuo  cha Mafunzo  ya Kijeshi  cha  TMA Meja  Jenerali  PP  Masao, Dk.  Magufuli  atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi la 57/15.

Alisema  Dk. Magufuli   atatunuku  kamisheni  kwa  maofisa  wanafunzi kundi hilo, katika  sherehe zitakazoanza  saa  mbili  asubuhi  chuoni hapo.

Meja  Jenerali  Masao   alisema  wageni   mbalimbali  kutoka  ndani  na nje  ya nchi  wanatarajiwa  kuhudhuria  sherehe  hizo.

Hii  ni  ziara  ya  kwanza  ya  Rais  Dk.  Magufuli   ambaye  pia ni  Amiri jeshi  Mkuu  wa  majeshi  ya ulinzi  na usalama,  kufika  mkoani Arusha na  pia  kutunuku  kamisheni, baada  ya  kuchaguliwa kushika  wadhifa  huo Oktoba, mwaka jana.

Katika  hatua nyingine,  wakuu  wa  wilaya  za  mkoa  wa   Arusha, zinazokabiliwa  na  tatizo  la  ugonjwa  wa  kipindupindu, wamewasilisha  taarifa ya hatua iliyofikiwa  katika  kukabiliana  na janga hilo,  inayoonyesha  kuwa  ugonjwa  huo  sasa  umepungua  kwa kiasi  kikubwa  na  uko mbioni  kumalizika  kabisa.

Wakuu  hao  ambao  ni Fadhili  Nkurlu  wa  wilaya  ya  Arusha  na Ernest Kahindi   wa  Longido, walisema  kwa  sasa  katika maeneo yao,  hakuna  wagonjwa  wapya  wa  kipindupindu  na wameendelea kuwataka  wananchi kuendelea  kuzingatia kamuni  za usafi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA