UN: MAELFU YA RAIA WAMEUAWA IRAQ
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq
Umoja wa
Mataifa unasema kuwa ghasia zinazowakumba raia nchini Iraq ni nyingi
huku takriban watu 18,800 wakiuawa kati ya tarehe mosi mwezi Januari
mwaka 2014 na 31 mwezi Oktoba mwaka 2015.
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi katika kipindi hicho kulingana na ripoti mpya ya UN.
Umoja wa
mataifa unawalaumu wanamgambo wa Islamic State kwa kuendesha ghasia na
kuwashikilia watumwa watu 3,500, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
Islamic state wanawashikilia watumwa 3,500 wengi wakiwa ni wanawake na watoto
Kamishna
mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Zeid Raad Al
Hussein anasema ripoti hiyo inaonyesha kile wakimbizi kutoka Iraq
wanatoroka wakati wanakimbilia Ulaya na maeneo mengine.
Ripoti
hiyo inatokana na mahojiano na wale waliohama makwao na ushuhuda wa moja
kwa moja kutoka kwa waathiriwa au wale walioshuhudia ukiukaji wa haki
za binadamu
Ripoti
hiyo inasema kuwa idadi ya raia waliouawa kati ya tarehe 1 Januari mwaka
2014 na Oktoba 31 mwaka 2015 ni 18,802 na waliojeruhiwa 36,245.
Umoja huo hata hivyo unatahadharisha kwamba idadi halisi huenda ikawa juu zaidi.
-BBC
0 comments:
Post a Comment