RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA PAMOJA NA KUFANYA UKAGUZI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye
amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Mufti na
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya
Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua
na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona wagonjwa
wao.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea
katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili
akitokea Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero zao
ndani ya muda mfupi ujao.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment