WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO NA TCRA JINSI YA KUGUNDUA SIMU FEKI
Kwa
kutambua nafasi waliyonayo waandishi wa habari katika kuelimisha jamii
kuhusu simu feki, Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imefanya semina
na waandishi wa habari visiwani Zanzibar ili kuwapa uwezo wa kutambua
simu feki ambazo kwa sasa zinaonekana kutumika kwa wingi nchini.
Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy,
akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu
Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa
matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo
umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima
Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko
Zanzibar.
Naibu
Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo
Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki
wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika
ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema
utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali unaweza kupiga namba
kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06# na utapata ujumbe wa Simu yako kwa
Mfano zitakuja tarakimu 15 mfano IMEI 12456789067654 Na Kupiga
15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama
huu Sony Mobile Communications AB -SONY C5555 – Xperia. huu ni mfano wa
kujua simu orijino.
Naibu
Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo
akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View
Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni
orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati
wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya
zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
Meneja wa
Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa
waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba
hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri
takribani waandishi wote simu zao orijino.
Naibu
Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo
akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo
baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa suimu siyo feki.
Mdau wa
habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na
uingiaji wa simu za kutoka ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano
huo.
Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa.
Ndg Issa
Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia Wananchi wa Vijiji na
zoezi hilo la ungunduzi wa simu feki na kuweza kuepuka na hasara hii,
wakati ikifika tarehe hiyo ya mwisho wa matumizi ya simu hizo feki.
Naibu
Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa wakati
wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya
Simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
Meneja
Mawasiliano TCRA Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa mkutano wao
na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya
simu feki ifikapo mwezi juni 2016.
Kaimu
Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif S Waziri
akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa neno la shukrani kwa
waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutowa elimu ya simu feki
kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli
ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar
Waandishi
wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa mafunzo ya kutambua
simu feki na Orijino uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar
Ocean View Kilimani Zanzibar.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot.
Zanzinews.com
0 comments:
Post a Comment