SERIKALI YALITAKA DIRA YA MTANZANIA KUKANUSHA TUHUMA DHIDI YA BALOZI OMBENI SEFUE
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu
taarifa za upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la
tarehe 29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue,
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw. Jamal Zuberi
na Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw. Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya
Habari (MAELEZO).
Baadhi ya
waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambane (ambaye hayupo katika
picha) iliyokuwa ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha
habari waliyoitoa hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu
wa Ombeni Sefue Ikulu”.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene ameutaka uongozi wa
Gazeti la Dira ya Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali
na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa
waliyoitoa katika toleo namba 404 la tarehe 29/02/2016 lenye kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli
wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika
uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala kuhusika na kampuni ya CRJE katika
utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma Oktoba 2007 kwani
katika kipindi hicho alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
“Serikali
inautaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo
kwa uzito ule uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga
wakidai wana ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo
vinavyohusika ikiwemo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema
Bw.Mwambene.
Aidha,
Bw.Mwambene amesema gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue alipigia chapuo Kampuni ya “UGG” iliyowahi
kuonyesha nia ya kujenga reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya
kweli na hakuna kampuni yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya
kujenga reli hiyo.
Mkurugenzi
aliendelea kusema kuwa gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati
alichokifanya Balozi Sefue ilikuwa ni kusoma matokeo ya uchunguzi ambao
hakuufanya yeye. Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi
iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi
huo.
Hata
hivyo serikali imewashauri wamiliki wa vyombo vya
habari,wachapishaji,wahariri, na waandishi wa habari wajikite kwenye
weledi na ukweli pia wafanye utafiti wa kina na kuandika mambo waliyo
na uhakika nayo.
0 comments:
Post a Comment