Friday 8 April 2016

ROBO FAINALI EUROPA::LIVERPOOL YAIBANA DORTMUND UGENINI



LIVERPOOL imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kwenda Robo Fainali ya UEFA Europa League baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini na Borussia Dortmund Uwanja wa Signal Iduna Park.

Liverpool's No 27 scored his sixth goal of the season with the help of a deflection to ensure the Reds led at the half-time interval
Na Liverpool inayofundishwa na kocha wa zamani wa Borussia, Jurgen Klopp ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Divock Origi dakika ya 36, kabla ya Mats Hummels kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48 katika mchezo ambao wenyeji Dortmund waliutawala zaidi lakini Liverpool iliwanyima nafasi ya kulikaribia lango lango kwa karibu huku ikifanya mashambulizi hatari langoni mwa Dortmund.
Sasa Liverpool itahitaji hata sare ya 0-0 nyumbani Uwanja wa Anfield Aprili 14 ili kusonga mbele.

Mfungaji wa bao la Liverpool, Divock Origi akiangalia mawinguni kushangilia baada ya kufunga 
Mignolet fails to get his right hand onto the ball as Hummels' header is directed towards the back of the Belgium international's net
Mats Hummels  akiipatia bao la kusawazisha Dortmund


Mechi nyingine za Robo Fainali ya michuano hiyo leo, Villarreal imeshinda 2-1 dhidi ya Sparta Prague, mabao yote yakifungwa na Cedric Bakambu dakika ya tatu na 63, huku la wageni likifungwa na Jakub Brabec dakika ya 49 Uwanja wa El Madrigal.
Sporting Braga imefungwa 2-1 nyumbani na Shakhtar Donetsk Uwanja wa Manispaa mjini Braga. Mabao ya Shakhtar yamefungwa na Yaroslav Rakitskiy dakika ya 44 na Facundo Ferreyra dakika ya 75, wakati la wenyeji limefungwa na Wilson Bruno Naval Costa Eduardo dakika ya 89.  
Athletic Club nayo imefungwa 2-1 nyumbani na Sevilla Uwanja wa San Mames. Mabao ya Sevilla yamefungwa na Timothee Kolodziejczak dakika ya 56 na Vicente Iborra dakika ya 83, wakati la wenyeji limefungwa na Aritz Aduriz Zubeldia dakika ya 47. Timu zote zinatarajiwa kurudiana Alhamisi ijayo, Aprili 14.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA