Showing posts with label USAJILI. Show all posts
Showing posts with label USAJILI. Show all posts

Friday, 25 November 2016

TSHABALALA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Image result for TSHABALALA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA
BEKI wa Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' tayari amesaini mkataba wa miaka miwili  wenye thamani ya Sh 40 milioni.

Beki huyo amesaini mkataba huo baada ya kufanyika makubaliano ya awali yaliyofanyika wiki iliyopita chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe ambapo jana mkataba wake ameusaini chini ya Rais wa Simba, Evans Aveva.

Kwa sasa Zimbwe Jr ni mali halali ya Simba baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali huku zingine zikimuhusisha kwenda Yanga.



"Tumemalizana sasa na Simba hivyo Zimbwe ni mali yao Wanasimba kwa miaka miwili, amepewa baraka zote na ninaamini atafanya kazi yake vizuri," alisema Meneja wake Herry Mzozo.

Friday, 22 July 2016

USAJILI MAJUU:: WIJNALDUM ATUA LIVERPOOL AKITOKEA NEWCASTLE UNITED


Katika kile kinachoonekana kuwa kocha wa Liverpool inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ,Klopp kujenga kikosi kikubwa na tishio ili kurejesha makali ya mabingwa hao wa kihistoria barani Ulaya, Liverpool imefanikiwa kumnasa mchezaji mahiri na machachari Georginio Wijnaldum toka  timu ya Newcastle United kwa ada ya pauni milioni 25 ambapo atavaa jezi namba tano.
 
Katika siku za karibuni Wijnaldum alikuwa akihusishwa na vijogoo hao wenye maskani yao jijini Liverpool na hatimaye tayari amekuwa mmoja wa wanafamilia hiyo.Wijnaldum aliyetua Uingereza msimu uliopita akitokea PSV Eindhove alijikuta akianza vyema na kuizoea ligi hiyo mashuhuri na kufanikiwa kuwa mfungaji bora katika timu ya Newcastle kwa kupachika mabao 11 katika michezo 38.

Katika uhamisho huu inasemekana licha ya kuwa Newcastle kushuka daraja ndio chanzo, lakini uhusiano kati ya kocha wa sasa Newcastle Rafa Benitez dhidi ya timu yake ya zamani Liverpool umekuwa sababu muhimu ya kukamilika.

"Binasfi nina msisimko kwasababu Liverpool ni klabu kubwa yenye historia kubwa na mara nyingi ni ndoto ya kila mchezaji kucheza kwenye  klabu kubwa kama Liverpool" Wijnaldum aliuambia mtandao wa Liverpoofc.com mara baada ya kutia saini.

 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa mchezaji huyu ambaye amekuwa wa sita kusajiliwa msimu huu na anaiongezea Liverpool uwanja mpana wa uchaguzi katika nafasi za kiungo mshambuliaji na atalazimika kusafiri kuelekea nchini Marekani ambapo Liverpool imeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.
 PICHA ZOTE NA Liverpoolfc.com

Monday, 4 July 2016

USAJILI::CHELSEA YAKAMILISHA USAJILI WA MICHY BATSHUAYI KUTOKA MARSEILLE

Timu ya Chelsea ya Uingereza imeanza kujiimarisha kwa kufanya usajili wa kwanza wa kumtwaa Michy Batshuayi kwa kitita cha paundi milioni 33 akitokea kwenye klabu ya Marseille kwa mkataba wa miaka mitano.

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji, alikuwa katika mazoezi hii leo baada ya klabu hizo mbili kukubaliana uhamisho huo mapema wiki hii, wakati Batshuayi akiwa kwenye michuano ya Euro 2016.

Timu nyingine za Uingereza za Crystal Palace na West Ham nazo zilikuwa zinamtolea macho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, hata hivyo Chelsea ilizizidi kete klabu hizo za Jiji la London.
                         Michy Batshuayi akionyesha jezi yake aliyokabidhiwa na Chelsea

Tuesday, 28 June 2016

USAJILI::LIVERPOOL YAKAMILISHA UHAMISHO WA SADIO MANE


Timu ya Liverpool imekamilisha kunasa saini ya raia wa Senegal Sadio Mane, 24, kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 34 kutoka Southampton.

Mane anajiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano, ikiwa ni mchezaji wa tatu kusaini na Liverpool katika majira ya joto baada ya kipa Mjerumani Loris Karius pamoja beki wa Mcameroon, Joel Matip.

Dau la nyota huyo wa Senegal ada yake itaongezeka na kufikia paundi milioni 36, na kuweza kumudu kupiku rekodi ya paundi milioni 35 ya Andy Carroll mwaka 2011 wakati alipokuwa mchezaji ghali kujiunga na Liverpool.
                                     Sadio Mane akisaini mkataba wa kujiunga na Liverpool 
                Sadio Mane akionyesha jezi aliyokabidhiwa katika timu ya Liverpool


Friday, 3 June 2016

MANCHESTER CITY YAMNASA GUNDOGAN

MATAJIRI wa jiji, Machester City wameamua kuanza kuijenga timu yao lakini kwa staili ya kuzibomoa timu nyingine huku wakianza na wajerumani Borussia Dortmund inayosuasua kurejesha makali yake.

City imeingia klabuni hapo na kumnyakua kiungo wao mahiri, Ilkay Gundogan ambaye amepewa mkataba wa miaka minne kwa ada ya uhamisho ya paundi 21 milioni.




Usajili wa kiungo huyu wa Ujerumani mwenye miaka 25 unakuwa wa kwanza kwa kocha Pep Guardiola tangu alipojiunga na City.

Gundogan atakosa michuano ya Euro pamoja na mechi za kwanza za msimu ujao wa ligi kufuatia kuumia goti mazoezini mwanzoni mwa mwezi Mei.

Tuesday, 31 May 2016

EDINSON CAVANI WA PSG AKANUSHA UVUMI KUHUSU REAL MADRID, MANCHESTER UNITED


MSHAMBULIAJI mahiri wa PSG ya Ufaransa, Edinson Cavani, amesema kuwa ataendelea kuitumikia timu hiyo na hana mpango wa kwenda Manchester United wala Real Madrid.
 Wakala wa mchezaji huyo, Claudio Anellucci alisema jana kuwa staa huyo wa Uruguay ameridhia kubaki hapo akiamini atapata mafanikio zaidi.


Thursday, 26 May 2016

ARSENAL YATAMBULISHA 'MIDO' MPYA GRANIT XHAKA KUTOKA BUNDESLIGA

Kiungo mpya wa Arsenal,Granit Xhaka akiwa amepozi na jezi ya timu hiyo baada ya kukamilisha usajili wa Pauni Milioni 35 kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.

UHAMISHO wa Granit Xhaka kutua Arsenal umeiva bada ya picha za mchezaji huyo akipozi kwa ajili ya kupigwa picha kwenye uwanja wa mazoezi ya klabu hiyo wa London Colney kuvuja. Kiungo huyo, 23, aliwasili London Ijumaa iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne na Arsenal na picha za Xhaka akiwa ametinga jezi mpya za Arsenal zitakazovaliwa msimu ujao wa 2016/17, ambazo pia bado hazijatambulishwa rasmi. 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswisi amekuwa akifuatiliwa na Arsene Wenger kwa miezi kadhaa na baada ya kuafikiwa kwa ada ya uhamisho ya pauni mil 33.3 na klabu  yake ya Borussia Monchengladbach, anakuwa mchezaji wa kwanza kuwasili Arsenal katika kipindi hiki cha usajili kinachotarajiwa kuwa ‘bize’. Mtumiaji wa ukurasa wa Twitter, Valon Demiri ambaye maskani yake ni Kosovo, aliposti picha hizo kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuripotiwa kuzipata kutoka kwa mtu wa karibu na Xhaka.

 Kiungo huyo ametua London na wazazi wake, kaka yake na mkewe kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kupozi kwa ajili ya picha kabla ya kutangazwa rasmi kwa usajili huo.



Tuesday, 24 May 2016

LIVERPOOL FC YAMNASA KIPA LORIS KARIUS KWA MKATABA WA MUDA MREFU






Mchaka mchaka wa usajili umeanza kupamba moto!!!Klabu ya Liverpool imetangaza rasmi kukamilika kwa usajili wa mlinda mlango Loris Karius  kutoka  klabu ya FSV Mainz 05 mwenye umri wa miaka 22 kwa mkataba wa muda mrefu mara baada ya kufuzu vipimo vya afya klabuni hapo.



Akizungumza na mtandao wa timu hiyo Karius alisema "Ni hisia nzuri sana na ni heshima kuichezea klabu kama hii.

Loris Karius

Kipa huyo amethibitishiwa kuvaa jezi namba moja ambayo hapo awali ilikuwa ikivaliwa na Brad Jones pamoja na wakongwe David James, Jerzey Dudek pamoja na Sander Westerveld.

Karius ambaye ameiwakilisha  Ujerumani katika ngazi ya U21 , alicheza mechi  34 za Bundesliga msimu uliopita , ambapo  hakuruhusu goli katika mechi tisa na kusaidia Mainz kumaliza ligi katika nafasi ya sita atajumuishwa  rasmi katika kikosi cha Liverpool Julai Mosi.

Karius anakuwa mchezaji mpya wa pili kuwasili Liverpool hadi sasa baada ya  Joel Matip kusajiliwa mapema mwaka huu na na alihitaji hitimisho la mkataba wake wa sasa na FC Schalke. 
-Liverpoolfc.com
Karius atajumuishwa  rasmi katika kikosi cha Liverpool Julai Mosi
Karius atajumuishwa  rasmi katika kikosi cha Liverpool Julai Mosi
Karius atajumuishwa  rasmi katika kikosi cha Liverpool Julai Mosi

Sunday, 22 May 2016

LIVERPOOL WAWINDA SAINI YA SERGIO RAMOS



MAJOGOO wa Jiji la London, wanapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia nyota wa Real Madrid, Sergio Ramos, laini wanalazimika kuweka dau la ziada mezani la pauni 24 milioni kwa ajili ya jembe hilo. Ramos amekuwa akihusishwana kujiunga na Liverpool katika usajili ujao wa dirisha la Januari, lakini Liverpool inabidi kupambna kwa ajili ya kiungo huyo ambaye pia anawaniwa kwa karibu na Manchester United. 

Jurgen Klopp akipeana mikono na beki  Ramos wakati akkifundisha Dortmund
United wanatajwa katika dili la kumfukuzia nyota huyo wa Real Madrid kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha Mashetani Wekundu hao. Lakini tarifa zinasema kuwa tayari kocha Jurgen Klopp ameshamaliza mazungumzo ya awali ya kiungo huyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kinachopambana kwa ajili ya kuirejesha klabu katika hadhi yake ya miaka ya awali. 


Awali, Liverpool waliweka mezani dau la pauni 15 mil. Kwa ajili ya Sergio Ramos kabla ya Madrid hawajaweka bayana kuwa dau la kiungo huyo ni 45 mil. Bado Liverpool wanakomaa na dau la awali lakini wakaweka bayana kuwa wanaweza wakaongeza kiasi cha pauni 2 milioni ili dili kufikia pauni 12 milioni. Ramos amekuwa katika kiwango bora katika kipindi cha miaka miwili hii na kuwa na uhakika wa kuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.


Saturday, 14 May 2016

LIVERPOOL YATANGAZA KUMUWINDA BEKI HUMMELS WA DORTMUND

KLABU ya Liverpool imeingia katika vita ya kumwania beki mahiri wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Mats Hummels. Habari zinasema kwamba kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameamua kuingia katika vita ya kumwania beki huyo kutokana na ukweli kwamba beki huyo sasa hana mapenzi tena ya kucheza katika klabu hiyo ya zamani ya mwalimu huyo.

Klopp amekaririwa akisema kwamba anataka kumsajili beki huyo kutokana na mahitaji ya sasa ya beki wa aina yake na kwamba haoni kama ni lazima beki huyo kwenda katika timu pinzani ya Bayern Munich. “Ni kweli kwamba mchezaji huyo ameonekana anataka kwenda Bayern lakini mimi pia nataka kuzungumza nae na kumsajili hapa Liverpool,” amesema Klopp. Mapema wiki iliyopita beki huyo ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na viongozi wa Ligi ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, Bayern Munich baada ya kukamilika msimu huu.


Mats Hummels amesema hana amani katika kikosi hicho na kwamba anataka kukatiza mkataba na kuangalia maisha mengine. Mapema wiki hii, mwenyekiti wa Bayern, Karl Heinz Rummenigge alifichua kuwa klabu hiyo ilikuwa tayari inafanya mazungumzo na nahodha huyo wa Dortimund kuhusu uhamisho.

 Dortmund imethibitisha katika taarifa kuwa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 27 ambaye ana mkataba hadi Juni, 2017 amewasilisha ombi rasmi la kutaka kuondoka. Kwa sasa Bayern haijatoa ofa na kuwa mchezaji huyo ataweza kuondoka tu ikiwa kwa kutolewa kiasi cha pesa kitakachokubaliwa.

 Hummels atajiunga na Mario Goetze aliyeondoka mwaka 2013 kwa kiasi cha euro milioni 37 na mshambuliaji Robert Lewandoswki aliyesaini mwaka 2014. Hata hivyo, kocha wa Liverpool amesema ni wakati mwafaka sasa kumsajili mchezaji huyo aisema kwamba yuko katika orodha ya wachezaji ambao anawataka kutoka Borussia alikotokea kabla ya kujiunga na Liverpool.


OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA