Monday 23 May 2016

MECHI MOJA TU!! KUAMUA SAMATTA KUCHEZA EUROPA LEAGUE


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo amecheza kwa dakika za 61, timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji Genk katika mchezo wa mchujo Ubelgiji kuwania kucheza michuano ya Ulaya.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent, Samatta alimpisha Mgiriki, Nikolaos Karelis baada ya kupigana kwa saa moja uwanjani bila bao. 

Na kwa sare hiyo, Genk sasa italazimika kushinda dhidi ya mshindi kati ya Charleroi na Kortrijk ili kupata tiketi ya kucheza Europa League kupitia mchujo wa mwisho.
Samatta leo amecheza mechi ya 16 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.

Katike mechi hizo, ambazo tisa ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA