Saturday 21 May 2016

MTU MWENYE SILAHA APIGWA RISASI NJE YA IKULU YA MAREKANI

Kikosi cha kumlinda rais wa Marekani, kimempiga risasi mwanaume mmoja nje ya Ikulu ya nchi hiyo, kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa Marekani.

Polisi wameliambia shirika la habari la ABC kwamba mwanaume huyo alionesha silaha katika kizuizi cha ukaguzi karibu na jengo la Ikulu na alipigwa risasi tumboni.

Kwa muda mfupi Ikulu ya Marekani ilifungwa baada ya tukio hilo la Ijumaa, lililotokea wakati rais Barack Obama akicheza mchezo wa gofu huko Maryland.

Mtu aliyepigwa risasi amepelekwa hospitali akiwa kwenye hali mbaya.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA