Wednesday 11 May 2016

NI MIUJIZA TU KWA MANCHESTER UNITED KUNUSA TOP FOUR MSIMU HUU


Manchester United goalkeeper David de Gea got a hand to the header but was unable to stop Reid from scoring the winner
Kipa mahiri wa Manchester United akijaribu kuuzuia bila mafanikio mpira ulioipa Westham goli la ushindi 
MANCHESTER United sasa inasubiri miujiza kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya England baada ya kukubali kichapo cha bao 3-2. Kabla ya mchezo wa huo wa kiporo uliochezwa Jumanne usiku kwenye dimba la Upton Park, United ilikuwa na  matumaini ya kumaliza katika nafasi ya tatu, lakini sasa imebakiwa na nafasi finyu ya kushika nafasi ya nne. 
Reid runs away with his West Ham team-mates in celebration after scoring the winner against Manchester United
Mfungaji wa bao la ushindi Winston Reid akiwaongoza wenzake kushangilia mara baada ya kupachika goli la tatu
United yenye pointi 63 sasa italazimika kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya AFC Bournemouth Mei 15 halafu iombe Manchester City yenye pointi 65 ifungwe na Swansea City, kinyume na hapo, klabu hiyo ya Old Trafford itajikuta ikiambulia nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao huku Champins League ikiota mbawa kwao. 

West Ham ilikuwa ya kwanza kufunga katika dakika ya 10 kupitia kwa Diafra Sakho bao lililodumu hadi mapumziko. Anthony Martial akaifungia United mabao mawili katika dakika ya 58 na 72 na kuifanya West Ham ikicharuke na kupata magoli yaliyokuja dakika ya 76 na 81 yaliyofungwa na Michail Antonio na Winston Reid.

MSIMAMO WA LIGI BAADA YA MECHI HII

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA