Monday 2 May 2016

SADIO MANE APIGA HAT-TRICK SOUTHAMPTON IKIICHAKAZA MAN CITY


Matumaini ya Manchester City kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya yapo kwenye hati hati baada ya Sadio Mane kuonyesha makali yake kwa kufunga mabao 3 yaani hat-trick na kuisaidia Southampton kushinda kiulaini mabao 4-2.

Alikuwa mchezaji Shane Long aliyefungua karamu ya magoli, na kisha Mane kuongeza la pili kwa shuti la umbali wa yadi 10, hata hivyo Manchester City walizinduka na kupata bao lililofungwa na Kelechi Iheanacho.

Mane tena akatikisa nyavu mara mbili ili kuihakikishia ushindi Southampton kwa kuwahi mpira wa kichwa wa Jose Fonte uliogonga mwamba na baadae kuunganisha pasi ya Dusan Tadic, kabla ya Iheanacho tena kuifungia Manchester City. 
                                      Sadio Mane akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
                          Kelechi Iheanacho akifurahia goli lake kwa kushukuru Mungu 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA