Tuesday, 14 June 2016

BRAZIL YAMTIMUA DUNGA "UKOCHA TIMU YA TAIFA"

BRAZIL imemfukuza kazi kocha Carlos Dunga baada ya matokeo mabaya kwenye michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani.

The Selecao wametolewa kwenye hatua ya makundi tu ya mashindano hayo baada ya kutoa sare na Ecuador na kufungwa na Peru, licha ya kushinda 7-1 dhidi ya Haiti.

Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa Corinthians, Tite, ambaye ataiongoza timu hiyo katika michuano ijayo ya Olimpiki nchini Brazil.

Dunga aliingia kwenye mashindano hayo akiwa katika wakati mgumu baada ya timu kucheza vibaya kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 na pamoja na matokeo mabaya ya Marekani, imesababisha kufukuzwa kwake. 

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA