EURO 2016::GRIEZMANN, PAYET WAIPATIA UFARANSA USHINDI WA JIONI
Mshambuliaji wa Ufaransa, Dimitri Payet akitimba kibendera cha kona kwa furaha baada ya kuifungia timu yake bao la pili dakika |
Ufaransa
imefanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika hapo kabla kwenye michuano ya Ulaya
baada ya kuichapa Ablania 2-0 huku magoli yote yakija baada ya dakika ya 90.
Griezmann anayekipiga na Atletico Madrid akifunga kwa kichwa goli lake hilo la dakika ya 90 |
Mshambuliaji wa Ufaransa aliyetokea benchi Antoine Griezmann akishangilia bao lake dakika ya 90 dhidi ya Albania Jumatano jioni |
Ilikuwa ni kama vile mechi hiyo ya Euro 2016
inamalizika kwa sare, lakini mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine
Griezmann aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kingsley
Coman akaifungia Ufaransa bao la kwanza dakika ya 90. Wakati Ufaransa wakiwa
bado hata hawajamaliza furaha ya bao hilo, mambo yakazidi kunoga pale Dimitri
Payet alipofunga goli la pili katika dakika za majeruhi.
Hii
ni mara ya pili mfululizo kwa wenyeji Ufaransa kupata bao la ushindi ukingoni
mwa mchezo, kwani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Romania, Dimitri
Payet alifunga bao la ushindi dakika ya 90 na kufanya mpira umalizike 2-1.
Katika mchezo huu, kocha Didier Deschamps aliwaanzishia
benchi Antoine Griezmann na Paul Pogba nafasi zao zikipelekwa
kwa Anthony Martial na Kingsley Coman kabla hawajaingizwa kipindi cha
pili.
Staa wa West Ham United Dimitri Payet akifunga goli la pili kwa ufundi wa hali ya juu |
Hana Bahati!!!Giroud anapiga mpira wa kichwa unaokwenda kugonga mwamba |
0 comments:
Post a Comment