EURO 2016::WALES, UINGEREZA ZATINGA HATUA YA MTOANO MICHUANO
Timu za taifa za Wales na Uingereza zimetinga hatua ya mtoano ya michuano ya Euro 2016 baada ya kukamilisha michezo yao ya mwisho ya kundi B, katika michuano hiyo inayofanyika nchini Ufaransa.
Katika mchezo wao wa jana usiku Wales wasioogopa kitu waliifunga Urusi magoli 3-0 na kuongoza kundi hilo, huku Uingereza ikishika nafasi ya pili baada ya kutoa sare tasa na Slovakia.
Wales waliandika goli la kwanza kupitia kwa Aaron Ramsey, na kisha Neil Taylor kupachika la pili kabla ya Gareth Bale kufunga la tatu, na kumfanya aongoze kwa kufunga magoli mengi katika michuano hiyo.
Mshambuliaji nyota Gareth Bale akiifungia Wales goli la tatu
Jamie Vardy akipiga ngumi mwamba wa goli kwa hasira baada ya kukosa goli
Wayne Rooney akionyesha kuchanganyikiwa baada ya goli kukoswa
0 comments:
Post a Comment