Tuesday 7 June 2016

RAIS MUSEVENI AMTEUA MKEWE, JANET MUSEVENI KUWA WAZIRI WA MICHEZO NA ELIMU

Janet Museveni, Mke wa Rais Yoweri Museveni na Waziri wa Michezo na Elimu wa Uganda
Janet Museveni, Mke wa Rais Yoweri Museveni na Waziri wa Michezo na Elimu wa Uganda
Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni amemteua mkewe, First Lady Janet Kataha Museveni kuwa Waziri wa Michezo na Elimu.
Kwa mujibu wa orodha ya Baraza Jipya la Mawaziri wa nchi hiyo, Janet Museveni anakuwa miongoni mwa viongozi 81 wanaounda baraza hilo.
Janet anachukua nafasi ya Jessica Alupo ambaye alikuwa Waziri katika wizara hiyo kabla ya uchaguzi wa Februari 18 mwaka huu ambapo Museveni aliibuka mshindi licha ya matokeo hayo kupingwa vikali na wapinzani wakiongozwa na Kiiza Besigye, daktari wa zamani wa Museveni kutoka chama cha FDC
Katika baraza lake jipya Museveni amechagua pia Mawaziri kutoka upinzani wakiwemo Betty Kamya ambaye amemteua kuwa Waziri anayehusika na kusimamia Jiji la Kampala. Pia amempa Evelyn Anite Wizara ya Ubinafsishaji.
Pia Rais Museveni amemfuta kazi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Fred Ruhindi na kumteua Byaruhanga William kuchukua nafasi hiyo. Pia amemuondoa aliyekuwa Waziri wa Afya, Dr.Elioda Tumwesigye na kumpa nafasi hiyo Acey Jane.
Pia Rais huyo mwenye umri wa miaka 71 na aliyesomea Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam, amewabakisha madarakani washirika wake wengi ambao wamekuwa naye madarakani tangu mwaka 1986 walipochukua nchi. Mawaziri hao ni pamoja na Tumukunde Henry (Ushushushu), Adolf Mwesigye (Ulinzi), Kahinde Otafiire (Sheria), Sam Kutesa (Mambo ya Nje), Jeje Odongo (Mambo Ya Ndani), Kirunda Kivejinja (Makamu Waziri Mkuu wa Pili) na Moses Ali Makamu Waziri Mkuu wa Kwanza).
Rais Museveni ni miongoni mwa marais wa Afrika waliodumu madarakani kwa miaka mingi zaidi. Akimaliza awamu hii ya Urais mwaka 2021 atakuwa amekalia kiti cha Urais wa nchi hiyo kwa miaka 35. Ni kiongozi wa chama kinachotawala cha National Resistance Movement(NRM). Miezi michache iliyopita Rais Museveni alitolewa macho na ulimwengu wa kimataifa baada ya kumpandisha cheo mwanae Muhoozi Kainerugaba kuwa Meja Jenerali katika jeshi la Uganda (UPDF). Muhoozi ni kamanda wa kikosi maalumu kilicho na Presidential Guard Brigade ambayo kazi yake kuu ni ulinzi wa Rais.
Orodha kamili ya Baraza La Mawaziri wa Museveni ni kama ifuatavyo;
H.E. the Vice President ─ HON. KIWANUKA EDWARD SSEKANDI
  1. Rt. Hon. Prime Minister ─ DR. RUHAKANA RUGUNDA
  2. 1st Deputy Prime Minister & Deputy Leader of Gov’t Business in Parliament─ GEN. MOSES ALI
  3. 2nd Deputy Prime Minister and Minister of East African Affairs ─ HON. KIRUNDA  KIVEJINJA
  4. Minister of Education and Sports ─ HON. MUSEVENI JANET KATAAHA
  5. Minister of Public Service ─ HON. MURULI MUKASA
  6. Minister of Trade, Industry & Cooperatives ─ HON. KYAMBADDE  AMELIA ANNE
  7. Minister of Internal Affairs ─ GEN. JEJE ODONGO
  8. Minister of Agriculture, Animal Industry & Fisheries ─ HON. SSEMPIJJA VINCENT BAMULANGAKI
  9. Minister of Finance and Economic Planning ─ HON. KASAIJA MATIA
  10. Minister of Foreign Affairs ─ HON. KUTESSA KAHAMBA SAM
  11. Minister of Health ─ DR. ACENG JANE
  12. Minister of Works and Transport ─ ENGINEER NTEGE AZUBA
  13. Minister of Lands,Housing & Urban Development ─ HON. AMONGI BETTY
  14. Minister of Water &Environment ─ HON. CHEPTORIS SAM
  15. Minister of Justice & Constitutional Affairs ─ MAJ. GEN.KAHINDA OTAFIIRE
  16. Attorney General ─ MR. BYARUHANGA WILLIAM (ADVOCATE)
  17. Minister of Defence and Veteran Affairs ─ HON. MWESIGE ADOLF
  18. Minister of Local Government ─ HON. BUTIME TOM
  19. Minister for Karamoja Affairs ─ HON. BYABAGAMBI JOHN
  20. Minister of Energy and Minerals ─ HON. MULONI IRENE
  21. Minister of Information, ICT & Communications ─ HON. TUMWEBAZE  FRANK
  22. Minister for Science, Technology and Innovation ─ DR. TUMWESIGYE ELIODA
  23. Minister in Charge of General Duties/Office of the Prime Minister ─ HON. BUSINGYE MARY KAROORO OKURUT
  24. Minister of Disaster Preparedness & Refugees ─ HON. ONEK HILARY
  25. Minister of Tourism, Wildlife & Antiquities ─ PROF. KAMUNTU EPHRAIM
  26. Minister for the Presidency ─ HON. MBAYO ESTHER MBULAKUBUZA
  27. Minister of Security ─ LT. GEN. TUMUKUNDE HENRY
  28. Minister without Portfolio ─ HAJJI NADDULI29. Minister for Kampala City Authority ─ HON. KAMYA BETTY
  29. Government Chief Whip – HON. NANKABIRWA SENTAMU RUTH
  30. Minister of Gender, Labour & Social affairs ─ HON. MUKWAYA JANAT
MINISTERS OF STATE:
Office of the President:
  1. Minister of State for Economic Monitoring ─ HON. KASIRIVU BALTAZAH ATWOKI
  2. Minister of State for Ethics and Integrity ─ HON. LOKODO SIMON
Office of the Vice President:
  1. Minister of State Vice President’s Office ─ HON. ONZIMA ALEX
Office of the Prime Minister:
  1. Minister of State for Relief and Disaster Preparedness ─ HON. ECWERU MUSA FRANCIS
  2. Minister of State for Northern Uganda ─ HON. KWIYUUCWINY GRACE
  3. Minister of State for Karamoja ─ HON. KIZIGE MOSES

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA