Tuesday 28 June 2016

TP MAZEMBE YAIZIBA YANGA KATIKA UWANJA WA TAIFA DAR



MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeshindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 toka kwa TP Mazembe kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga walianza mchezo huo kwa kasi  na kufanya mashambulizi ya haraka langoni mwa Mazembe lakini ulinzi wa Wakongomani uliokuwa chini ya Salif Coulibaly ulikuwa imara.

Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu Obrey Chirwa na Juma Mahadhi walionesha kandanda safi nakushangiliwa na maelfu ya wapenzi wa mabingwa hao waliohudhuria mechi hiyo lakini walishindwa kuisaidia timu yao kupata ushindi.

Dakika ya 33 Yanga walifanya shambulizi kali langoni mwa Mazembe mpira uliopigwa na beki Vincent Bossou ulitoka nje huku mshambuliaji Mtanzania wa Mazembe, Thomas Ulimwengu akiwapa wakati mgumu vijana hao wa Jangwani.

Kiungo Marveille Bope ndiye aliyepeleka kilio kwa watoto wa Jangwani baada ya kufunga goli pekee dakika ya 75 kufuatia mabeki wa Yanga kuzembea kuondoa mpira hafifu wa adhabu ndogo uliopigwa na Jean Kasusula kabla haujamkuta mfungaji.

Winga mpya wa Yanga Juma Mahadhi alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumizwa na Kasusula na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya dakika ya 65.

Yanga iliwatoa Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na nafasi zao kuchukuliwa na Godfrey Mwashiuya pamoja na Matheo Anthony.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka Yanga katika mazingira magumu baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo huku ikitakiwa kusafiri hadi Ghana kucheza na Madeama City wiki mbili zijazo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA