Monday 27 June 2016

USAJILI:LIVERPOOL WAMALIZANA NA SOUTHAMPTON, MANE KUFANYA VIPIMO JUMATATU



Liverpool imepiga hatua kubwa katika harakati za kumsajili winga machachari wa kutoka Southampton kwa dau la pauni milioni 30 ambapo sasa yamebaki mazungumzo binafsi na mchezaji huyo ambaye anatarajiwa kufanya vipimo vya afya katika viunga vya Melwood siku ya Jumatatu.


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa akivutiwa sana na aina ya uchezaji wa Mane na ndiyo sababu ya kufanya mpango wa kumsajili kwa kitita kikubwa cha pesa. Mane atakuwa mchezaji wa tano kutua Liverpool akitokea Southampton katika kipindi cha miaka miwili ambapo alitanguliwa na  Rickie Lambert, Adam Lallana, Dejan Lovren pamoja na beki Nathanael Clyne.

Ujio wa Mane unazidi kufungua mlango kwa mshambuliaji wa Ubeligiji Christian Benteke ambaye ameshindwa kumshawishi Klopp kumfanya kuwa chaguo la kwanza huku timu kdhaa zikimtolea udenda.

Endapo Mane atatua Anifield anatarajia kuongeza kasi katika  safu ya ushambuliaji ya Liverpool huku  ikiongezewa makali na  mshambuliaji Danny Ings ambaye amerejea kutoka majeruhi ya muda mrefu.
Mane alimaliza msimu uliopita akiwa amepachika magoli 11 katika michezo 37 ya ligi kuu England akiwa na klabu ya Southampton.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA