Saturday 18 June 2016

UTALII WA NDANI WAZIDI KUPATA MASHIKO ,WASOMI CHUO KIKUU SMMUCo WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

Simba dume  akiwa anaunguruma 
Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi 
Na Dickson Mulashani

Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngoro ngoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana humo.
Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro

Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho”  alisema.
Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake 

Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater

Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi
Watalii wakiwa katika harakati za kupata picha ya simba

 


Katika ziara hiyo ambapo wasomi hao walizuru eneo lenye umaarufu wa aina yake la “Ngoro ngoro Crater” waliweza kujionea mimea,ndege na wanyama mbali mbali wakiwemo samba, kifaru, nyumbu,pundamilia , fisi, nyati swala pamoja na ndege kama tai, cranes pamoja na flamingo.


Wito : ziara hii iwe chachu kwa jamii ya kitanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuvitembelea vivutio vinavyopatikana maeneo mbalimbali nchini mwetu ili kuwa sehemu ya kukuza sekta ya utalii na kujivunia upekee wetu kama nchi iliyobarikiwa.

Wanafunzi hao wakiwa katika eneo la view point sehemu ambapo watalii huweza kuona eneo la crater kwa upande wa juu 

PICHA ZAIDI


Ngiri na mbweha wakinywa maji katika moja ya mabwawa ya asili katika eneo la crater



Fisi wakiwa wamejilaza kando kando ya maji ili kupunguza joto mwilini wakati wa mchana

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA