Saturday 2 July 2016

EURO 2016::WALES YAITUMIA UBELGIJI KAMA NGAZI NA KUTINGA NUSU FAINALI


Timu ya taifa ya Wales imetinga nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 kwa mara ya kwanza baada ya kupambana kiume na kuifunga Ubelgiji kwa jumla ya magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa huko Lile, Ufaransa.

Alikuwa Radja Nainggolan aliyeifanya Ubelgiji kuongoza kupata goli kwa shuti kali la yadi 25, hata hivyo kapteni wa Wales Ashley Williams alisawazisha kwa mpira wa kichwa kufutia mpira wa kona na kufanya kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya 1-1.

Wales walipata furaha pale Hal Robson-Kanu, mshambuliaji asiye na klabu alipopachika goli na kuwafanya kuongoza kwa magoli 2-1, huku Sam Vokes aliyetokea benchi akipachika goli la tatu.

Kwa ushindi huo Wales sasa watakutana na Ureno katika mchezo wa nusu fainali, itakayowakutanisha washambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.
                              Hal Robson-Kanu akipiga mpira uliozaa goli la pili kwa Wales
    Sam Vokes akiwa juu baada ya kuupiga mpira kwa kichwa ulioandika goli la tatu kwa Wales

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA