SEHEMU YA PILI::NAMNA YA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO
Visababishi Vya Msongo Wa mawazo
Kuna vitu vingi vya kimazingira au kimsukumo vinavyoweza
kusababisha uwe na msongo wa mawazo, vitu hivi hutwa “stressors”. Nafikiri
msomaji wangu unafikiri kuwa kila kitu kinachokuletea msongo wa
mawazo (Stressor) ni kibaya, kama kubanwa sana na kazi au mahusiano mabaya
ya kimapenzi. Stressor ni kitu cho chote kinachodai matumizi ya juu ya
uwezo na nguvu zako za mwili. Inawezekana kuwa kikawa kitu kizuri tu, kama
kuoa/kuolewa, kununua nyumba, kujiandaa kwenda chuoni au hata kupandishwa cheo
kazini.
Msongo wa mawazo unaweza kutokana na fikra zako binafsi mbali na
sababu hizo ambazo ni za nje ye mwili wako. Unaweza kuwa na msongo wa
mawazo kutokana na kukifikiria na kukiogopa kitu ambacho kinaweza kutokea
au ambacho hakiwezi kutokea au tu ukawa na mawazo chanya kuhusu maisha.
Ni kitu gani kitakupa msongo wa mawazo na kipi hakitakusumbua
inategemea sana na namna wewe mwenyewe binafsi utakavyokichukulia kitu
kilicho mbele yako, kitu hicho hicho ambacho wewe kinakusumbua, kinaweza
kuwa ni burudani kwa mtu mwingine. Kuendesha gari katika foleni toka Mbezi
kuingia kazini kwako Posta kunaweza kuwa kero kubwa kwako, wakati kwa
mwingine ni fursa yake ya kupata muziki mwororo asubuhi.
Vitu ambavyo vinasababisha msongo wa mawazo ni pamoj na:
·
Mabadiliko ya maisha
·
Kazi au shule
·
Matatizo katika mahusiano
·
Matatizo ya kifedha
·
Kubanwa na shughuli nyingi
·
Watoto na familia
·
Wasiwasi wa muda mrefu
·
Tabia ya kuona kila kitu ni kibaya
·
Kupenda yasiyowezekana
·
Kutaka kila kitu kiwe sahihi (kikae
juu ya mstari) kila wakati
·
Kutopenda kushauriwa au kubadilika
kutokana na hali halisi
·
Kujidharau mwenyewe kwenye mazungumzo
Msongo wa mawazo unaotokana na majibizano na rafiki yako, au ule
unaotokana na msongamano wa magari au wa kuwa na ratiba ndefu na ngumu ya
shughuli ni tofauti na msongo wa mawazo wa kuwa na majukumu mengi katika
familia. Msongo wa mawazo unaokwenda kwa muda mrefu ni hatari kwa afya na
huweza kuvuruga vitu vingi katika mwili wako ukaishia na magonjwa kama ya
high blood pressure, upungufu wa kinga za mwili, kiharusi, ukosefu wa
uwezo wa kuzaa au kuzalisha na kuzeeka haraka. Msongo wa mawazo wa muda
mrefu huweza kusababisha mfadhaiko (Depression).
USIKOSE SEHEMU YA TATU
KAMA ULIMISS SEHEMU YA KWANZA >>BOFYA HAPA<<
0 comments:
Post a Comment