Wednesday 20 July 2016

YATAMBUE MADHARA YA KUTUMIA VIPODOZI

Ni kweli vipodozi hukufanya uonekane vizuri (Mzuri), Unukie vizuri, kama ni mzee basi uonekane angalau kijana. Lakini unapaswa kujua kuwa ukitumia sana hukuletea madhara. Kibaya zaidi kuna baadhi ya watu hawawezi kujiamini kuwa wanamuonekano mzuri au wanavutia bila kutumia vipodozi. Jua kwamba maranyingine vipodozi hivi hutangazwa kuwa vimewekwa mchanganyiko ambao haupo kwenye vipodozi husika. Na haya ni madhara au matatizo yatokanayo na matumizi makubwa ya vipodozi.

1. MAUMIVU YA KICHWA
Hii hutokea endapo utakaa na "make-up" kwa mda mrefu. Kisayansi imeweza kuthibitishwa kuwepo kwa uhusiano kati ya vipodozi vipakwavyo juu ya ngozi na maumvu ya kichwa. Kujipaka "make-up" usoni huongeza uwezekano wa kukumbwa na kipanda uso ambacho huambatana na kizunguzungu, uchovu, kichefuchefu na kutapika.
Hivyo basi kama utajipaka vipodozi usoni (Make-up) basi usikae navyo mda mrefu na pia usipendelee vipodozi vikali.
2. HUONGEZA UWEZEKANO WA WA KUPATA SARATANI (CANCER)
Vipodozi vingi vya siku hizi huwa na machanganyiko ambao unaweza kusababisha saratani za aina mbali mbali ikiwemo saratani ya matiti, saratani ya ngozi na saratani ya damu. Pia "Lipstick" ina madini ya alumini (aluminum) ambayo hukusabashia upungufu wa damu (anaemia). Bidhaa nyingi zina mchanganyiko wa madini kama vile zinc oxide, BHA, barium sulphate n.k ambayo hupelekea kufeli kwa baadhi ya viungo kama vile ini na figo. Bahati mbaya haya makampuni yasambazayo hizi bidhaa wanafanya juu chini bidhaa zao zionekane hazina madhara

3. MADHARA KATIKA VIUNGO VYA UZAZI
 Imezoeleka kuwa wanawake ndo watumiaji wakubwa wa vipodozi basi wao ndio wapo katika hatari kubwa ya kupatwa na tatizo hili. Vipodozi vinavyopakwa kwenye ngozi na vile vya kuondoa harufu (deodorants) vina uhusiano na viungo vya uzazi na pia husababisha kutokuweza kuzalisha ( infertility) kwa hiyo unapaswa kuwa makini kwa hiyo usitumie make-up na vipodozi vyovyote mara kwa mara.

4. HULETA MZIO (ALLEGY)
Asilimia kubwa ya vipodozi huleta mzio. Kuna aina nyingi za mzio ambazo huletwa na utumiaji wa vipodozi uliopitliza. Kemikali nyingi zilizo katika bidhaa za kufanyia make-up zinaweza kukuletea madhara katika ngozi, macho na nywele.
Parabens (Michanganyiko ambayo huwekwa ili kufanya vipodozi visaribike, kemikali hizo kitaalamu ni kama vile ethyl-paraben, butyl-paraben, isopropyl-paraben n.k) imeripotiwa kusababisha kuja kwa mzio (allegy) kama ngozi kuwasha, kuleta mabaka na madoa katika mwili.

5. HULETA MATATIZO YA MACHO
Vitu vya kpendezesha macho inajumuisha kuweka kope bandia, kupaka wanja kupitlizaa, au kupaka vitu ili kope zionekane vizuri pamoja na make-up huweza kusababisha kope zisiote au kunyonyoka kwa kope pia huweza kuleta maambukizi kama macho kuwa mekundu (redness) au kuwashaWanja huzalisha wadudu (Bacteria waitwao  pseudomonas aeruginosa) inapokaa kwa mda mrefu.
Macho ni mojawwapo ya kiungo muhimu katika mwili wa binadamu kwa hiyo usihatarishe macho yako kwa kuyafanya yawe mazuri kupitiliza.

Kwa hiyo kama utajipaka vipodozi usoni (Make-up) basi usikae navyo mda mrefu na pia usipendelee vipodozi vikali. Vitakuletea matatizo ya kchwa, macho, matatizo katika viungo vya uzazi (Ikiwemo kushindwa kuzaa au kuzaa mtoto mwenye matatizo), pia matatizo mzio (allegy) endapo lipstick ikiingia tumboni aidha kwa kumezwa au kuingia na chakula.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA