Monday 8 August 2016

ARSENAL YAIZAMISHA MANCHESTER CITY KWA MAGOLI 3-2 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI


Alex Iwobi, Theo Walcott pamoja na Chuba Akpom wameizamisha Manchester City kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Katika mchezo huo Sergio Aguero aliifanya Manchester City iongoze manamo dakika ya 30 kwa kuachia shuti la karibu kufuatia krosi iliyopigwa na Raheem Sterling. Alex Iwobi alisawazishia Arsenal kwa shuti la kuzungusha lililomshinda kipa Joe Hart.

Arsenal iliongoza tena zikiwa zimebakia dakika 17 mpira kumalizika baada ya Theo Walcott kukimbilia pasi ya Sanchez na kuunyanyua mpira juu ya kipa Hart. Chuba Akpom aliifungia Arsenal goli la tatu, kabla ya Kelechi Iheanacho hajafunga goli la pili la Chelsea.
                                             Alex Iwobi akiifungia Arsenal goli la kusawazisha
                                       Sergio Aguero akiifungia Manchester City goli la kwanza
           Kelechi Iheanacho akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa ulioiandikia Manchester City goli la pili

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA