ATABAKI:::LEICESTER CITY YATANGAZA KUMBAKIZA MAHREZ KIKOSINI
Leicester City inaamini kuwa Riyad
Mahrez ataendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu mpya unaoanza wikiendi hii
kufuatia mazungumzo ya kina na mkurugenzi wa klabu hiyo Jon Rudkin. Arsenal
imekuwa ikihusishwa kwa karibu na usajili wa Mahrez lakini mabingwa hao wa
England hawana dhamira ya kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Algeria mwenye
umri wa miaka 25. Kiwango cha Mahrez kimemkuna
Arsene Wenger lakini kocha wa Leicester Claudio Ranieri ameendelea
kusisitiza kuwa nyota huyo haondoki.
0 comments:
Post a Comment