LIVERPOOL YAANZA VYEMA UGENINI KWA KUICHAPA ARSENAL 4:3
![]() |
Kocha wa Liverpool Klopp akisherekea kwa mtindo wa aina yake pamoja na wachezaji wake mara baada ya kupata bao la nne |
Timu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imeanza vyema harakati za kurejea katika nafasi yake ya kupigania ubingwa baada ya kuichapa timu ya Arsenal kwa goli 4 kwa 3.
![]() |
| Kipa wa Liverpool Simon Mignolet akiokoa mchomo wa penati uliopigwa na Theo Walcott |
![]() |
Kipa pamoja na walinzi wa Liverpool wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kuangalia mpira uliopigwa na Theo Walcott kuandika bao la kwanza la mchezo
|
Katika mchezo huo ambao ni kama kila timu ilijigawia dakika 45 ikiwa zile za kwanza zilikwenda kwa wenyeji Arsenal na kupata bao la kuongoza kunako dakika ya 30 likipachikwa na Theo Walcott ikiwa ni dakika moja tangu alipokosa penati baada ya mlinda mlango wa Liverpool Mignolet kuokoa jahazi na dakika ya 45 Coutinho alisawazisha kwa bao kali kupitia mkwaju aliopiga kufuatia mpira wa adhabu.
![]() |
Kipa wa Arsenal mkongwe Peter Cech akishuhudia mchomo mkali uliopigwa na Coutinho ukiingia wavuni na kuisawazishia Liverpool
|
Liverpool walianza kipindi cha pili kwa kasi sana na kupata mabao matatu ya haraka ndani ya dakika 19 za kwanza yakifungwa na Adam Lallana katika (49) na Coutinho tena katika dakika ya 56 kabla ya winga machachari aliyesajiliwa msimu huu Sadio Mane kuitikisa ngome ya Arsenal na kupachika bao la 4 katika dakika ya 63.
![]() |
| Beki Calum Chambers akiipatia Arsenal bao la tatu juu ya walinzi wa Liverpool |
Ikiwa imedhaniwa vijana wa Kocha Wenger wamekata tamaa, mchezaji aliyeingia katika kipindio cha pili aliwainua tena mashabiki kwa kufunga goli la pili dakika ya 65 na dakika kumi baadae beki Calum Chambers akaiandikia Arsenal bao la tatu ambalo pia halikuweza kuwaokoa na kipigo hicho.
![]() |
| Shabiki wa wenyeji Arsenal akiwa amejishika kichwa kuonesha hali ya kukata tamaa
Picha na DAILY MAIL UK
|







0 comments:
Post a Comment