Monday 8 August 2016

MANCHESTER UNITED YAANZA KWA KUTWAA NGAO YA HISANI,KOCHA JOSE MOURINHO AMZAWADIA VAN GAAL

Kocha Jose Mourinho ameanza vyema akiwa na Manchester United kwa kutwaa kikombe baada ya Zlatan Ibrahimovic kufunga goli la kichwa la dakika za mwisho na kuibuka na ubingwa wa ngao ya hisani katika dimba la Wembley.

Katika mchezo huo ulioishia kwa magoli 2-1 dhidi ya Leicester City, Jesse Lingard ambaye alifunga goli la ushindi katika kombe la FA, wakiwa na kocha Louis van Gaal, alipachika goli la kwanza baada ya kuwatoka mabeki wanne.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester walijibu mapigo baada ya Marouane Fellain kutoa pasi mbovu ya nyuma iliyompa fursa mshambuliaji hatari Jamie Vardy kuchomoka na kuachia shuti lililomshinda kipa David de Gea.

Hata hivyo mchezaji aliyesajiliwa majira ya joto Ibrahimovic, 34, aliizamisha Leicester City zikiwa zimebakia dakika saba tu mpira kumalizika aliporuka juu na kuunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Antonio Valencia na kumshinda kipa Kasper Schmeichel.

Baada ya mchezo huo kuisha kocha Jose Mourinho alikaririwa akisema kuwa ushindi huu anaupeleka kama zawadi kwa mtangulizi wake aliyeondoka Old Traford mwishoni mwa msimu Mholanzi Loius Van Gaal. 
             Jesse Lingard akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza
                 Zlatan Ibrahimovic akipiga mpira kwa kichwa ambao ulizaa goli la pili
            Zlatan Ibrahimovic akiangalia mpira alioupiga kwa kichwa ukijaa wavuni

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA