Sunday 18 September 2016

ARSENAL YAENDELEA KUITAFUNA HULL CITY


Mchezaji Alexis Sanchez amefunga mara mbili wakati Arsenal wakipanda katika nafasi nne za juu za msimamo wa Lifgi Kuu ya Uingereza baada ya kuwafunga Hull City magoli 4-1.

Kikosi hicho cha kocha Arsene Wenger kilipata goli la kwanza wakati Sanchezi alipofunga kwa kuugonga mpira uliopigwa na Alex Iwobi na kuubadilisha muelekeo katika dakika ya 17.

Sanchez alikosa penati pale Jake Livermore alipocheza rafu na kutolewa kwa kadi nyekundu, hata hivyo baadaye Theo Walcott alifunga goli na Sanchez na Granit Xhaka nao kufunga.

Goli pekee la Hull City waliocheza wakiwa kumi kwa muda mwingi baada ya Livermore kutolewa lilifungwa na Robert Snodgrass kwa mkwaju wa penati.
             Alexis Sanchez akiachia shuti lililozaa goli lake la pili katika mchezo huo
                                                    Theo Walcott akifunga goli katika mchezo huo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA