Sunday 18 September 2016

MANCHESTER CITY YAITANDIKA BOURNEMOUTH 4:0 NA KUENDELEA KUJIKITA KILELENI


Manchester City imeendeleza ushindi wa nane katika michuano yote kwa msimu huu, baada ya hii leo kupata ushindi laini wa magoli 4-0 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Etihad.

Katika mchezo huo Kevin de Bruyne aliwapatia vinara hao wa Ligi Kuu ya Uingereza goli la kwanza kwa shuti la adhabu la chini baada ya Jack Wilshere kufanyiwa madhambi.

City walioutawa mchezo huo walifanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa Kelechi Iheanacho na Raheem kuongeza la tatu kabla ya Ilkay Gundogan kufunga kwa utulivu goli la nne.
                  Kelechi Iheanacho akianguka chini baada ya kupiga mpira uliojaa wavuni
                   Raheem Starling akipiga mpira ulioandika goli la tatu la Manchester City

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA