Wednesday 14 September 2016

UEFA::MESSI ATUPIA 3 BARCELONA IKIIADHIBU CELTI 7:0

Mshambuliaji nyota Lionel Messi amefunga hat-trick yake ya sita katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Barcelona ikiisambaratisha Celtic magoli 7-0.

Mchezaji huyo raia wa Argentina alifunga goli lake la mapema dakika ya tatu, na kisha kuongeza jingine dakika ya 27 kabla ya Neymar kuongeza la tatu katika kipindi cha pili.

Andres Iniesta alifunga goli la nne na Messi kuongeza la tano na kisha Luis Suarez akamalizia karamu ya magoli kwa kufunga goli la sita na la saba.
                                        Lionel Messi akiangalia mpira alioupiga ukijaa wavuni 

                             Kipa akiufuata bila ya mafanikio mpira uliopigwa na Neymar

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA