Thursday 22 September 2016

REMIX::MANCHESTER UNITED USO KWA USO NA MAN CITY KOMBE LA LIGI


Katika droo ya kombe la ligi nchini Uingereza iliyochezeshwa usiku huu Manchester United imejikuta ikitakiwa kuvaana na mahasimu wao Manchester City katika uwanja wa Oldtraford mwezi ujao,
Itakumbukwa kuwa  mapema mwezi katika mechi za ligi kuu England msimu huu Manchester United ilikubali kipigo cha goli 2;1 toka kwa Manchester City katika uwanja huo wa Old Trafordo hivyo basi mchezo huu maarufu kama Manchester derby unatoa nafasi kwa mashetani wekundu ama kulipa kisasi au kuendelea kuwa vibonde  kwa vijana wa Guardiola.

Pamoja na mechi hiyo katika raundi hii ya nne kuna mechi kali kadhaa ambapo Lierpool wakiwa wenyeji pale Anfield watakuwa wenyeji wa Totenham Hotspurs huku kukiwa na London derby kati ya Westham United watakapoikaribisha Chelsea.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA