Saturday, 29 October 2016

MANCHESTER UNITED YASHIKWA SHATI, CITY,ARSENAL, LIVERPOOL ZAZIDI KUPIGANA VIKUMBO KILELENI


MANCHESTER United imebanwa mbavu na Burnley kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa ligi uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.

United walitawala sana mchezo huo kwa kulishambulia lango la Burnley lakini hawakuweza kupata bao ambapo mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic alikosa nafasi nyingi za kufunga.

Manchester United 0-0 Burnley, PLAYER RATINGS: Heaton stars as Ibrahimovic flopsMwamuzi Mark Clutternberg alimtoa kwenye benchi Kocha Jose Mourinho baada ya kuongea maneno yakukosoa maamuzi ya refarii huyo huku pia akimlima kadi nyekundu kiungo Ander Herrera kutokana na kudhamiria kumkanyaga mchezaji mmoja wa Burnley.

Kikosi cha United kilichoanza leo ndicho kilichoisambaratisha Man City katikati ya Juma lililopita kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kombe la Capital One na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.

Matokeo mengine ya michezo ya ligi hiyo iliyochezwa leo ni kama ifuatavyo;

Sunderland 1-4 Arsenal
Middlesbrough 2-0  Bournemouth
Tottenham Hotspur 1-1 Leicester City
Watford 1-1 Hull City
West Bromwich 0-4 Man City

Crystal Palace  - 4 Liverpool  

MSIMAMO WA LIGI BAADA YA  MECHI ZA JUMAMOSI

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA