Sunday 2 October 2016

STOKE CITY WAIKOMALIA MANCHESTER UNITED KATIKA DIMBA LA OLD TRAFFORD


Stoke City wamelazimisha kuondoka na pointi moja katika dimba la Old Trafford baada ya Joe Allen kutumia vyema makosa ya kipa David de Gea na kufanya matokeo kuwa sare ya goli 1-1.

Baada ya kipa Lee Grant kuokoa kwa ustadi michomo kadhaa ya Manchester United kabla ya mapumziko, United walifanikiwa kutikisa nyavu kupitia mchezaji aliyetokea benchi Anthony Martial kwa mpira wa shuti la kuzungusha.

Goli hilo lilionekana kuwa ni pigo kubwa kwa Stoke City ambao walionekana kuwa sio tishio kabisa, lakini kipa De Gea alishindwa kudaka shuti la Glen Johnson huku naye Jon Walters shuti lake likigonga mwamba kabla ya Allen kuisukumizia mpira wavuni.
      Anthony Martial akipiga mpira ambao ulizaa goli la kwanza kufungwa katika mchezo huo
                     Mpira uliopigwa na Joe Allen ukielekea kujaa wavuni na kusawazisha goli 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA