Tuesday 29 November 2016

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA TIMU YA SOKA CHAPECOENSE YA BRAZIL YAANGUKA LEO ASUBUHI NCHINI COLOMBIA

Mabaki ya ndege
Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.


Maafisa wanasema watu sita wamenusurika. huku chanzo cha kuanguka  Ndege hiyo kikielezwa ni kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme huku taarifa zikisema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.

Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, amesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura huku hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.
Sambamba na hilo hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA