OFISI YA WAZIRI MKUU YAPOKEA MIFUKO 1000 YA SERUJI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAAFA KAGERA
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Amsons-Camel Bw. Salim A.Salim baada ya kukabidhi msaada wa Mifuko 1000 ya Seruji kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi la Kagera Novemba 09, 2016 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim (kushoto) akitoa maelezo ya msaada wa mifuko 1000 ya Seruji kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) walipofika katika Ofisi yake Dar es Salaam Novemba 09, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (katikati) akipeana mkono wa shukrani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim wakati wa kuwasilisha msaada wao wa mifuko 1000 ya Seruji kwa waathirika wa maafa Kagera, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Amsons-Camal Bw. Ghalib H. Ghalib. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment