Saturday, 12 November 2016

POGBA, DIMITRI PAYET WAIBEBA UFARANSA KATKA USHINDI DHIDI YA SWEDEN


Wachezaji Paul Pogba na Dimitri Payet wamecheka na nyavu wakati Ufaransa ikiathimisha mwaka mmoja wa mashambulizi la Paris kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sweden, katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.

Kabla ya kuanza mchezo huo uwanja mzima ulikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka watu 130 wahanga wa mashambulizi hayo yaliyotokea Jijini Paris Novemba 13, 2015. Emil Forsberg aliifanya Sweden iongoze katika kipindi cha pili kwa goli la mpira wa adhabu.

Hata hivyo mchezaji wa Manchester United Paul Pogba alisawazisha haraka goli hilo na kisha baadaye Ufaransa ilipata goli la pili kupitia kwa Dimitri Payet katika dakika ya 65 na kuifanya iongozi kwa tofauti ya pointi tatu katika kundi lao.
                  Paul Pogba akiuangalia mpira alioupiga kwa kichwa ukielekea kutinga wavuni
        Dimitri Payet akipiga mpira ulioenda kujaa wavuni na kuiandikia Ufaransa goli la pili

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA